Huyu ndiye mwanamuziki mwanaume aliyejibadilisha Jinsia na kuwa mwanamke.



Mwanamke huyu  kwa jina akijulikana kama  Titica, amekuwa ni gumzo kubwa nchini Angola.
 Siku chache zilizopita UNAIDS ilimpa heshima  mwanamke huyu aliyejibadili jinsia kuwa  Balozi wake.

Alizaliwa Luanda kama Teca Miguel Garcia,  akiwa muimbaji na mchezaji, Titica alibadili  maumbile yake miaka minne iliyopita mara
 baaada kufanya upasuaji wa maziwa  nchini Brazil.

Sasa, akiwa na miaka 26, Titica amekuwa  kioo cha Angola kwa aina ya muziki anaoufanya
 wenye mchanganyiko wa miondoko ya rap na
 techno unaojulikana kama “kuduro”.

Akiongea na BBC mwaka jana, akiwa kwenye  kwenye utengenezwaji wa video ya wimbo wake unaotamba sasa uitwao Olha o Boneco, wimbo
 ambao amemshirikisha muimbaji mashuhuri wa  muziki aina ya kizomba aitwaye Ary, Titica  alisema amefanikiwa kukabiliana na  vikwazo vyake.

“Shukrani kwa Mungu, nina furaha sana,  imechukua muda kufika hapa na imehusisha  mambo mengi ya kujitolea ila asante Mungu,
 kila kitu kinakwenda sawa kwangu.
 
Nilikuwa nikipigwa mawe, nimekuwa nikipigwa  na kumekuwa na vikwazo vingi vya kisheria dhidi
 yangu, watu wengi walionyesha hilo. Kuna miiko  mingi sana,”.

Licha ya miiko hiyo, bado Titica anaonekana  kuwa hana upungufu wa mashabiki huku wengi  wakiwa wanavutiwa zaidi na muziki wake kuliko
 jinsia yake.

Credit: Jovin Bachwa Blog.


About Unknown

Zanzibar is Our Home Town, lets embrace her and enjoy her fruits while we Last.

Toa Maoni kupitia Face book / Comment Using Using Facebook

No comments:

Leave a Reply


Top