Yanga na Simba wanapofurahi Pamoja

Mashabiki wa Simba na Yanga katika sehemu mbalimbali za jiji la Dar es salaam Jana wamepokea kwa kishindo promosheni ya Nani Mtani Jembe inayoendeshwa na bia ya Kilimanjaro Premium Lager nchi nzima kwa siku 75 ili kuleta mwamko katika utani wa jadi kati ya mashabiki hao.

Kampeni hiyo ilipokelewa kwa kishindo baada ya wafanyakazi wanaoitangaza kampeni hiyo wakiwa na msafara wa magari kutembelea maeneo mbalimbali ya jiji hususani yale ambayo ni maarufu kwa kuwa na mashabiki au makundi maarufu ya ushabiki kama vile Wakali wa Terminal, Vuvuzela Tandale, nk pamoja na vijiwe na matawi ya Simba na Yanga na kutoa burudani na maelezo ya kushiriki pamoja na kuitambulisha rasmi mtaani kampeni hiyo ya aina yake.

Baadhi ya wafanyabiashara katika soko la Tandika wilaya ya Temeke walisema kuwa kampeni ya Nani Mtani Jembe imeleta mwamko mkubwa sana katika utani wa jadi uliopo kati ya mashabiki wa Simba na Yanga na pia wanaamini itasaidia kuwaleta karibu zaidi mashabiki pamoja na kuibua mashabiki wapya.
 “Jonathan Assey alisema “Nimeanza kushabikia Yanga tangu nikiwa na miaka 14 lakini sijawahi kuona tukio lolote kubwa la kusisimua namna hii ambalo ni mahususi kwa ajili ya mashabiki, hivyo nawashukuru Kilimanjaro Premium Lager kwa kutukumbuka sisi mashabiki na kutuletea hii kampeni”.





Mashabiki wa Simba na Yanga wakiwa wanacheza kwa furaha jana wakati wa maandamano maalum yaliyofanywa kuitangaza Nani Mtani Jembe inayoendeshwa na Kilimanjaro Premium Lager kwa mashabiki wa jiji la Dar es salaam. Msafara huo utatembelea maeneo mbalimbali ya jiji la Dar es salaam kwa siku tatu kuitambulisha kampeni hiyo  na kutoa elimu namna ya kushiriki. 




Msafara wa magari yakipita katika Barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam jana kuitangaza kampeni ya Nani Mtani Jembe inayowashindanisha mashabiki wa Simba na Yanga kuzipa shavu timu zao kupitia kampeni hiyo inayoendeshwa na Kilimanjaro Premium Lager. Msafara huo utatembelea maeneo mbalimbali ya jiji la Dar es salaam kwa siku tatu.

About Unknown

Zanzibar is Our Home Town, lets embrace her and enjoy her fruits while we Last.

Toa Maoni kupitia Face book / Comment Using Using Facebook

No comments:

Leave a Reply


Top