Polisi Pemba wapewa kompyuta, printa.

RPC Zanzibar.
Jeshi la Polisi Kitengo cha Dawati la Jinsia na Watoto Mkoa wa Kaskazini Pemba, limeahidi kukabiliana na vitendo vya udhalilishaji wanawake na watoto kwa kuboresha utendaji wake kupitia teknolojia ya kompyuta ya kuhifadhi matukio yanayotokea ndani ya mkoa huo.
Mkuu wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai wa Pemba, Juma Sadi alisema hayo wakati akipokea msaada ya kompyuta moja na printa zenye thamani ya Sh1.9 milioni zilizotolewa na Shirika la Action Aids Pemba hivi karibuni.
Sadi amesema vifaa hivyo vitakuwa ni msaada mkubwa kwa jeshi hilo katika kuhifadhi kumbukumbu za matukio mbalimbali na itakuwa rahisi kwa Polisi wa Upelelezi kuwatambua wahalifu pindi kunapotokea vitendo vya uhalifu.

About Unknown

Zanzibar is Our Home Town, lets embrace her and enjoy her fruits while we Last.

Toa Maoni kupitia Face book / Comment Using Using Facebook

No comments:

Leave a Reply


Top