Kimemsibu Muuza chapati, Usitukane Wakunga.....!!!


Anachokifanya anti hapo pichani, si kigeni, anatengeneza chapati. Anti huyu huamka saa kumna1 asbuhi, akoke moto, akande unga, atengeneze chapati, akaange. Hii ni kazi yake ya kila siku. Anti huyu amekuwa akipika chapati miaka mi5 sasa, hivyo hivyo akiziuza kwa shida, maana kinachofuatia hapo ni kusubiri wateja, chapati moja TSH 200/=. Bahati, hapo jirani yake akahamia mdada mmoja, akawa mteja wake, anachukua chapati mbili kila siku anaenda nazo kazini. Mara yule mdada akaanza chukua nne, mara 8 mara 10, mara
akaweka oda ya chapati 100 kila siku. 

Mama akawa hana jasho la kuuza tena, yaani dada wa watu akifika tu analamba chapati 100 anasepa. Kwa vile anachukua 100, mdada akaomba awe anauziwa moja kwa 150/=, anti akaona inalipa, anti akakubali, mdada sasa akawa anachukua chapati 200 kila siku. Mama wa watu akaanza fuatilia kisirisiri, mdada anapeleka wapi? 

Kumbe yule dada anazichukua, anaenda nunua foil, anazifunga kwenye foil anauza Ofisini kwao na ofisi ya shosti yake jirani. Anauza moja Mia Tano. Mama kugundua, kaanza vimba, mara ananuna nuna, mara siku nyingine atengeneze 40 tu, mara aseme leo nnaumwa, mara leo nna oda kubwa dadaangu siwezi kukupa, basi akendelea hivyo ili mdada ashindwe. Mdada akamwambia anti naona mie niache tu. Anti akafurahi. Kesho yake anti akatengeneza 200 akamtuma mtoto wake wa kike akaziuze ktk zile ofisi mbili, unajua nini, aliuza 10 tu. Yule mdada alishaangaliaga plan B, anachukua kwa mama mwingine, tena anazipata kwa mia mia, sasa ana ofisi ya 3 anasaplai chapati 300 kila asbuhi. Kwa huyu mama mwingine jiko halikuwa zuri akampa jiko zuri na hotpots.

Tujifunze:

1. Ukiuza Samsung yako laki, aliyenunua akaenda uza milioni, piga kimya, haikuhusu!

2. Ukiona mwenzako anauza sana, usidhanie basi nawe unaweza anza chako ka kile ukauza sana, hujui siri ya biashara yake

3. Anti angetakiwa afurahie mafanikio ya mdada, fursa ya huyu anti ni kuomba masalahi, walau sasa aombe dada anunue kwa shs 170, ajenge hoja na sio kumfanyia visa.
4, HUYU MDADA ANANUNUA FOIL KUFUNGA CHAPATI
6. Endeleeni wenyewe....7.... 8..... 9.....


Source: mashughuli blog.

About Unknown

Zanzibar is Our Home Town, lets embrace her and enjoy her fruits while we Last.

Toa Maoni kupitia Face book / Comment Using Using Facebook

No comments:

Leave a Reply


Top